
76 views
Katika Makala ya Jasho Langu Riziki Yangu ambayo hukujia kila siku ya Jumanne saa moja asubuhi; leo hii , tunakupeleka katika eneo la Eshikulu kwenye Wadi ya Sinoko katika Kaunti ya Kakamega mahali ambapo chini ya jua kali na vumbi linalopaa angani, kuna akina mama jasiri wanaovunja mawe ili kujipatia riziki. Hawa ni mashujaa wa kimya, wanaochonga kesho bora kwa mikono yao wenyewe. Kila pigo la nyundo si kazi tu, ni mapambano ya maisha. Kila jiwe linalopasuka ni ishara ya matumaini, matumaini ya kulisha familia, kusomesha watoto, na kusimama imara katikati ya changamoto. Mwanahabari wetu Luke Wasike amezungumza na akina mama hawa, ambao licha ya kazi ngumu wanaendelea kusukuma gurudumu la maisha bila kukata tamaa. Edited & Uploaded by Razaq Malik Graphics by John Muthui ©2025 Radio47 Cape Media Limited