
97 views
Katika Kitengo cha Kero Lako, wiki hii tunaangazia ongezeko la vurugu na ghasia katika mikutano ya kisiasa hasa ya upinzani. Matukio ya hivi karibuni ni vurugu zilizoshuhudiwa mjini Kisii siku ya Jumatatu wakati wa ziara ya viongozi wa upinzani wakiongozwa na Fred Matiangi wakati kundi la vijana lilipojaribu kuwazuia kuingia mjini huku wananchi waliokuwa na hamaki wakijaribu kuwakabili. Pia usisahau vurugu zilizoshuhudiwa Kitengela wakati wa mkutano wa Linda Mwananchi ukiongozwana Edwin Sifuna. Mwanahabari wetu Kombo Alphayo amezungumza na wananchi kuhusiana na suala hili. Edited & Uploaded by Razaq Malik Graphics by John Muthui ©2025 Radio47 Cape Media Limited