
96 views
Katika Kitengo cha Kero Lako, siku ya Jumanne wiki hii, jopo kazi linaloangazia dhulma za kijinsia humu nchini lilimkabidhi Rais William Ruto ripoti yake kuhusiana na tatizo hilo huku ikipendekeza litajwe kuwa Janga la Kitaifa ili raslimali nyingi zielekezwe katika kulikabilii. Hata hivyo kinachowakera wananchi ni kilichobainishwa kwenye ripoti hiyo kwamba kuna mrundiko wa kesi takriban elfu nane zinazohusiana na dhulma hizo. Mwanahabari wetu, Amina Rahman ameliangazia swala hili kwa kuzunguza na wakazi wa Kajiado ambapo katika siku za hivi karibuni visa vya wanawake waliouliwa kwenye visa vinavyoaminika kuwa vya dhulma za kijinsia katika mahusiano vimekuwa vikiripotiwa. Edited & Uploaded by Razaq Malik Graphics by John Muthui ©2025 Radio47 Cape Media Limited