
128 views
Katika makala ya Tashtiti Ya Wiki, kwa mara nyingine tena, mahanjam ya soka yamenoga. Matokeo ya Kenya dhidi ya Angola yameamsha makeke ya Wakenya wapenda kandanda. Hii ndiyo raha ya kambumbu eti, lakini Harambee stars watawezana na timu ya Morocco? Chairman Mwakideu ameiweka katika sala. Na suala la kujenga kanisa ikulu linaonekana kutofikia kikomo kwenye vinywa vya watu kadhaa. Profesa kwa upande wake, anadai kiongozi mwema ni yule anayenyeyekea, lakini kama kawaida, Wamunyoro ni yuleyule. Mwanahabari wetu Allan Wetungu anatupambia makala haya. Edited & Uploaded by Razaq Malik Graphics by John Muthui ©2025 Radio47 Cape Media Limited