Hatutagombea viti vya Kabuchai, Matungu na Machakos, Jubilee yatangaza rasmi

  • | K24 Video
    Chama cha Jubilee kimetangaza kutowania nyadhifa za ubunge Matungu na Kabuchai na pia useneta wa Machakos. Katibu wa chama hicho Raphael Tuju amedai kuwa watashirikiana na vyama vyenye maadili kama yao katika chaguzi hizo. Kuhusiana na ugavana wa Nairobi. Tuju amesema wanasubiria uamuzi wa korti na mwelekeo kuhusu uchaguzi huo.