Wahudumu wa afya waachwa bila suluhu huku serikali kuu na serikali za kaunti zikikosa kukubaliana

  • | K24 Video
    Serikali za kaunti na serikali kuu zinaonekana kubebeshana mzigo wa utatuzi wa mgomo wa wahudumu wa afya. Baraza la magavana linadai kuwa moja ya suluhu ya utatuzi wa vuta nkuvute iliyopo ni kuongezwa kwa bajeti ya kaunti. Kwa sasa hatahivyo serikali za kaunti zinadai hakuna pesa za kuwalipa na pia hawakuhusishwa na muafaka kati ya serikali kuu na wahudumu wa afya.