
169 views
#TafakariYaShangilia na Amani Aila Kitabu: Warumi 16:17-21. Ndugu zangu, nawasihi mjihadhari na wote wanaoleta mafarakano na vipingamizi kinyume cha mliyopokea. Waepukeni. Kwa maana watu kama hao hawamtumikii Bwana Kristo, bali wanatumikia tamaa zao wenyewe. Kwa kutumia maneno matamu ya kudanganya, hupotosha mioyo ya watu wanyofu. Kila mtu amesikia juu ya utii wenu na nimekuwa na furaha kwa ajili yenu. Lakini napenda muwe na hekima katika mambo mema na bila hatia katika mambo maovu. Na Mungu wa amani hatakawia kumponda shetani chini ya miguu yenu. Neema ya Bwana wetu Yesu iwe pamoja nanyi. Amen!