Hassan Wario ameachiliwa huru baada ya kulipa faini.

  • | K24 Video
    Aliyekuwa waziri wa michezo Hassan Wario ameachiliwa huru baada ya kulipa faini ya shilingi milioni 3 na laki 6, alizotozwa na mahakama baada ya kuhukumiwa kuhusiana na sakata ya michezo ya Olimpiki. Wario alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka 6 gerezani au faini ya shilingi milioni 3 na laki 6 kwa kupatikana na hatia pamoja na mwenzake stephen soi ambaye amepewa kifungo cha miaka 12 gerezani iwapo hatalipa faini ya shilingi milioni 105 nukta 5.