
27,081 views
11 Oct 2021
Download or listen online: https://mdundo.com/song/2166861 Performers: Kwaya ya Mt. Cesilia Parokia ya Mirerani Publisher: Verony Productions Ltd. Composer: J. B. Manota Copyright ©Verony Productions Ltd. (Tunaishi pamoja kwa amani ee ndugu yangu, Kama jumuiya moja, kwa pendo la Mungu *2) Ona, {Tumeunganishwa (sote) Kwa pendo lake Muumba, Sasa, kwa nini tufarakane Kwa mambo yatutengayo na Mungu }*2 Ugomvi kati yetu unatoka wapi, Mbona sisi sote ni watoto wa Baba mmoja Kwa nini tugombee mali za dunia Tukumbuke pendo lake Mungu, tuondoe tofauti zetu We baba nawe mama mwagombea nini, Mbona mwasahau ahadi yenu siku ya ndoa Ugomvi wenu unaathiri watoto Kumbukeni pendo lake Mungu, muondoe tofauti zenu Makasisi, watawa mwatafuta nini, Mbona mwasahau ahadi nazo nadhiri zenu Ubinadamu mbona unawatawala Kumbukeni pendo lake Mungu, mmkabidhi maisha yenu, Ugomvi wa kidini unatoka wapi, Mbona sisi sote ni raiya wa taifa moja, Kubagua kabila, rangi ni kwa nini, Tukumbuke pendo lake Mungu, tuondoe tofauti zetu Sasa enyi vijana mwatafuta nini, Mbona matendo yenu mengi ni chukizo kwa Mungu, Hamuheshimu wazazi na Mungu wenu, Kumbukeni pendo lake Mungu, mmrudieni Mungu wenu.