
35,828 views
8 Jun 2020
Performers: St. Joseph's Catholic Choir Kyalilini Producer: Verony Productions Ltd. Copyright ©Verony Productions Ltd. COMPOSER: Chris Kitema Twende kwake Bwana, Bwana Mungu wetu, Kwa unyenyekevu, tumuombe muongozo, Ni mwenye huruma, na fadhili nyingi, Atatubariki na kutujalia. Nitazame mimi, mwanako mnyonge, Nimezama kwenye lindi hili la dhambi. * 2 Ona jinsi mwovu, mwovu shetani, Amenizunguka na kunikanganya. * 2 Nayo imani yangu inayumbayumba, Niongoze Bwana nikae imara. * 2 Ulimwengu una vishawishi vingi, Teknologia, ufisadi mwingi. * 2 Sisi wana wako, twakimbia kwako, Tuhifadhi Mungu kwenye pendo lako. * 2 Mungu Baba yetu, tupe kupendana, Kupewapenda hata maadui zetu. * 2 Kwa huruma yako, tujalie uzima, Utupe uzima, ule wa milele. * 2