
57,300 views
20 Oct 2020
Performers: St. Joseph's Catholic Choir Kyalilini Producer: Verony Productions Ltd. Copyright ©Verony Productions Ltd. COMPOSER: Chris Kitema Nimezawadiwa mapaji yale ya mbinguni, Ndipo naja kwako Yesu uliye mwema kusema asante, Mema yako mengi ambayo we wanijalia, Sina budi kukushukuru na kukusifu, unipe neema. 1. Mwili wako na damu yako umenishibisha, Ni chakula cha roho zetu hutupea nguvu, Dhambi zangu waziondoa pia kuziosha, Wanishangaza mimi wako, hunitia nguvu. 2. Umenipa uhai wako na pumzi za bure, Ninaimba nikikusifu kwa furaha tele, Nitaruka angani mimi ili nikusifu, Na kuruka kama ndama kwa furaha tele. 3. Umenishibisha kwa neno, neno takatifu, Ukanipa pia mwongozo maishani mwangu, Umenipa pia kupenda maadui zangu, Ukanijalia kuishi kwa amani yako. 4. Ewe Yesu mwana wa Mungu kwa upendo wako, Ulinionyesha upendo kunifia mimi, Kwa mateso yako makali ulinikomboa, Toka utumwani mwa dhambi mimi nashukuru. 5. Ewe Bwana fadhili zako zadumu milele, Kwa uaminifu wako wewe ulinikomboa, Sauti nzuri wanijalia ili nikusifu, Neema zako umenijalia mimi nashukuru.