
76,312 views
18 Sep 2020
Performers: Christ the King Cathedral Choir - Bungoma Producer: Verony Productions Ltd. Copyright ©Verony Productions Ltd. COMPOSER: Joseph Shomaly Jogoo amewika sasa asubuhi na mapema {mapema} Amkeni watu wote njooni tumwimbie Muumba wa vyote *2 Tunyanyue mikono, ishara ya kumsifu Mungu, Tumshukuru Mungu kwani katuamsha salama. *2 1. Wanyama wote wa bondeni, ndege, samaki baharini, Na kila kinachotabaa, imbeni sifa zake Mungu. Mifugo yote ifugwayo, hata ile ya misituni, Imbeni sifa zake Mungu ametuamsha salama. 2. Moyo wangu unafurahi, mwili wangu waburudika, Ninapotaja jina Yesu, mkombozi wa roho yangu. Ninafurahia kuimba, ninafurahia kucheza, Ninamsifu Mungu wangu, ameniamsha salama. 3. Baba nakuomba bariki maisha niishio mimi, Niishi vile upendavyo na si vile ninavyopenda. Bariki na wazazi wangu, bariki na watoto wangu, Bariki familia yangu, na watu wote wabariki.