
161,460 views
16 Sep 2020
Performers: St. John Kusyomuomo Catholic Choir Producer: Verony Productions Ltd. Copyright ©Verony Productions Ltd. COMPOSER: Nichodemus Mwithi 1. Katika safari ya duniani, Maisha yanapojawa na hofu, Unapozama kwa shida na dhiki, Kumbuka Mungu wako yuko hai. {Tazama juu aliko Bwana, Uone pendo la moyo wake, Kumbuka Mungu wako yuko karibu nawe, Simama eeeeee muite Yesu, Rafiki kweli, nyakati zote.} x2 2. Umejaribu bila kufaulu, Uyafanyayo hayawezekani, Unapodhani yote yamekwisha, Kumbuka Mungu wako yuko hai. 3. Marafiki wako wamekutenga, Wamethibitisha wewe hufai, Washindwa mbona kifo chakawia, Kumbuka Mungu wako yuko hai. 4. Wasema huna mbele wala nyuma, Ulimwengu umekugeukia, Dunia kamwe haikuhitaji, Kumbuka Mungu wako yuko hai.