
33,163 views
4 Sep 2020
Performers: St Paul's Students' Choir - University of Nairobi Producer: Verony Productions Ltd. Copyright ©Verony Productions Ltd. COMPOSER: Joseph Shomaly Je? Je? Ni nani aliyesadiki habari hii tuliyoleta Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani? Maana alikua mbele zake kama mche kama mche mwororo {Na kama} kama mzizi katika nchi kavu Alidharauliwa na kukataliwa na watu Mtu mwenye huzuni nyingi ajuaye sikitiko X 2 1. Ni kama mtu ambaye watu humficha uso Aliyedharauliwa, hakuhesabiwa kitu Hakika kayachukua, na masikitiko yetu, Amejitwika huzuni, huzuni, huzuni yetu. 2. Lakini tulidhania, yeye kuwa amepigwa Ya kuwa yeye kapigwa kapigwa yeye na Mungu Bali alijeruhiwa, yeye kwa makosa yetu Alichubuliwa yeye, pia kwa maovu yetu. 3. Adhabu amani yetu, ilikuwa juu yake, Kwa kupigwa kwa sisi, sisi sote tumepona Sisi ni kama kondoo, kondoo tumepotea Tumegeukia njia, kila mtu njia yake.