
14,197 views
22 Dec 2019
Ni wimbo wa Krismasi, na heri ya mwaka mpya. Mwokozi amezaliwa, na dunia inafurahia Masiya aliyetabiriwa atazaliwa pangoni Bethlehemu, amekuja mwana wa Mungu mkombozi wa ulimwengu, mfalme mtawala, mfalme wa amani na Mungu mwenye nguvu. #Christmas #Noel #MasihaAjaye MASIHA AJAYE Je, wewe ndiwe Masiha (ndiwe yule) yule tunayemtarajia, (Wewe) Je, wewe ndiwe ujaye (na nguvu) mwenye uweza kutukomboa? Je, wewe ndiwe Masiha (ndiwe yule) yule waliyetuahidia, (Au) Je, bado yupo mwingine (ajaye) tupaswaye kungojea? K I I T I K I O sop / alto { Umekuja, kwetu mpole kabisa, Umevua, utukufu nguvu fahari, Kajivika, ubinadamu kabisa, Umekuja, ulimwenguni dhaifu, Makusudi, wewe utuokoe sisi } *2 tenor/bass { Umekuja mtoto, u mpole kabisa, Na umevua ukuu, utukufu fahari, Ukajivika unyonge, wa mwanadamu kabisa, Na umekuja tuliko, tungali dhaifu, Kwa makusudi, wewe utuokoe sisi } *2 M A S H A I R I 1. Leo limetimia, lile andiko la manabii, Kwamba bikira atachukua mimba, Na kumzaa mtoto wa kiume, na kumuita Emanueli! 2. Amejishusha mno, humu pangoni Betilehemu, Alimolala mchanga na mnyonge, Kusudi tumfikie bila woga, nani amuogopaye mtoto? 3. Wachungaji kondeni, na mamajusi wa mashariki, Na watu wa pande zote za dunia, Wakusanyika wanamsogelea, wote wamsujudia mtoto! mtunzi: Martin Mutua Munywoki Tazama pia nyimbo nyingine za Christmas kama Malaika kaleta noeli ya kwanza, lala kitoto cha mbingu, anakuja mtawala, wachungaji wakaenda kwa haraka, tumeiona nyota mashariki, leo yametimia, amezaliwa Masia Yesu Kristu, tazama bikira, jongeeni wakristu, zanena, kengele zasikika, furaha duniani, itengenezeni njia, leo tumepewa mtoto Mwokozi, n.k, tunawatakia krismasi njema na mwaka mpya wenye mafanikio