Halaiki ya watu kuzuiliwa kukongamana kwenye sherehe za Mashujaa uwanja wa Gusii hapo kesho

  • | K24 Video
    Baada ya saa chache tu, sherehe za Mashujaa zitaanza, zikifanyika wakati Nchi bado inapigana na janga la Corona. Sherehe hizo zitakazofanyika  katika uwanja wa Gusii Kaunti ya Kisii zimetajwa kuwa tofauti na za hapo awali kufuatia pigo la COVID-19. Huku kaunti hiyo ikianadaa sherehe hizo kwa mara ya kwanza kabisa. Kufuatia hilo, mikakati mbali mbali imewekwa, mojawapo ikiwa ni kuzuia halaiki kukongamana.