Mpango wa kusafirisha wanawake wajawazito usiku kupunguza vifo vya akina mama wajawazito| Siha Yangu

  • | K24 Video
    Wakati Serikali ilitoa amri ya kutotoka nje ilikudhibiti maambukizi ya virusi vya COVID-19, wanawake wajawazito, walikuwa miongoni mwa wale walioathirika pakubwa. Kwa mujibu wa Daktari Jemima Kariuki, alishuhudia idadi ndogo ya wale waliozuru vituo vya afya, huku waliofika hospitalini wakiwa katika hali maututi. Hapo ndipo alianzisha mpango wa kuwasafirisha wanawake wajawazito usiku kutoka makwao kufika katika vituo vya afya bila malipo.