2 waliokufa kwenye maandamano Kitengela walipigwa risasi

  • | Citizen TV
    3,810 views

    Sasa imebainika kuwa watu wawili waliofariki kwenye maandamano eneo la Kitengela wiki iliyopita waliuwawa kwa kupigwa risasi kichwani. Kulingana na mpasuaji wa maiti wa serikali Daktari Peter Ndegwa, mwandamanaji mwingine aliyefariki wakati wa maandamano katika eneo la Mlolongo alifariki baada ya kupigwa kwa kifaa butu kichwani. Na kama anavyoarifu Gatete Njoroge, familia za waathiriwa wawili ambao hapo awali walinakiliwa kama ambao walifariki kufuatia ajali wanadai haki wakiitaka serikali kuwachukulia hatua maafisa wa usalama waliowafyatulia risasi wapendwa wao.