
42 views
Mzazi mmoja eneo la Jomvu, kaunti ya Mombasa, anazuiliwa na polisi kwa madai ya kumkataza mwanawe kufanya mtihani wa kitaifa kufuatia utata kuhusu nambari ya usajili wa mtihani, maarufu kama index number. Kwa mujibu wa Celina Chirchir mkuu wa polisi Jomvu mzazi huyo amedai mwanawe alipewa nambari ya mtihani ya 666 anayodai inahusishwa na ushetani. Ililazimu wasimamizi wa shule anayosomea mtoto huyo kuwasiliana na maafisa wa polisi waliofika hadi nyumbani na kumtia mbaroni mzazi huyo huku mwanae akipelekwa kufanya mtihani wake. #Amacheni #Mulembefm