Ripoti ya BBI kupokewa rasmi katika Ikulu ndogo ya Kisii

  • | K24 Video
    Rais Uhuru Kenyatta na Kiongozi wa ODM, Raila Odinga hii leo katika Ikulu ndogo ya Kisii wamepokea rasmi ripoti ya BBI. Rais Kenyatta amewataka wakenya kuisoma ripoti hiyo kwani inahusu maisha ya wakenya huku akisema kuwa ripoti hiyo hainuwii kumlenga mtu yeyote wala jamii. Raila odinga kwa upande wake amedokeza kuwa kamati ilijumuisha maoni ya wakenya kutoka pembe zote za nchi na kuwa maswala yaliyopewa kipaumbele na ripoti hiyo yatashughulikiwa.