
187 views
Video inayosambaa mitandaoni inamuonyesha mwanamume mmoja akimwagia petroli sehemu za nje za gari lake katika kituo cha Shell Westview jijini Nairobi. Tukio hilo lililotokea Jumatano usiku limezua maswali kuhusu usalama na hatari zinazoweza kusababishwa na matumizi yasiyo sahihi ya mafuta katika vituo vya kujaza petroli.