
2,588 views
4 Mar 2014
IMANI UFUNGUO WA MIUJIZA YAKO NI IMANI PEKEE IWEZAYO KUTUFANYA TUFURAHI MAHALI AMBAPO TULIPASWA KUHUZUNIKA Stephano akipigwa mawe hakuona mawe bali alielekeza macho yake mbinguni akamuona Yesu akiwa ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Una majaribu? Usihuzunike tizama mlango wa kutoka kwenye majaribu yako kwani Mungu anasema pamoja na majaribu au mateso yetu, Yeye ataweka na MLANGO wa kutokea. Stephano Alipoona mlango wa kutokea aliwasamehe waliokuwa wakimpiga mawe kwani utukufu wa kule alikokuwa akienda ulizidi maumivu ya kupigwa mawe. Yacheke majaribu yako na wasamehe wanaokutesa kwani utukufu mbele yako ni mkuu kuliko majaribu yako. " Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali; ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo. Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu, katika kuupokea mwisho wa imani yenu, yaani, wokovu wa roho zenu. - 1 Petro 1:6-9"