
621 views
8 Nov 2026
EDWIN KAMALA - WANIWAZIA MEMA Unaweza usielewe unayopitia leo, lakini usiwe na shaka na mema ambayo Mungu ameyaandaa kwa ajili ya kesho yako. Mawazo yake kwako ni mawazo ya amani, si ya mabaya; ni ya kukupa tumaini na kwa wakati ujao uliojaa baraka. Wimbo uliochochewa na YEREMIA 29:11 (Inspired by Jeremiah 29:11) Waniwazia mema ni wimbo unaobeba ujumbe wa Imani, Tumaini, na Uhakika katika ahadi za Mungu. katika safari ya maisha, tunapitia nyakati za furaha na huzuni, mafanikio na changamoto. Kuna wakati hali tunazopitia zinatufanya tushindwe kuelewa kesho yetu. Lakini katikati ya yote hayo, tunapaswa kukumbuka kuwa Mungu ana mipango mema kwa ajili yetu. Anatuwazia mema. Hata pale ambapo hatuelewi kinachoendelea, Mungu bado anajua mwisho wa safari yetu. Mawazo yake kwetu ni ya amani, tumaini, na maisha yajayo yenye kusudi, Wimbo huu ni ukumbusho kwamba tusikate tamaa, tusipoteze imani wala kuacha kumtumainia Mungu. Yeye hajatusahau. Wakati wake ni mkamilifu na ahadi zake hazishindwi. Hujui kesho yako itakuwaje, lakini Mungu unamjua na ndiye anayeishikilia kesho yako. Ikiwa wimbo huu umekugusa moyo wako: Like video hii Share na uwapendao zaidi wapate kujua Mungu anawawazia mema Acha maoni yako kuwabari wengine Subscribe kwa nyimbo zaidi za Gosple. Mungu akubariki. Endelea kuwa na imani, maana bado Mungu anakuwazia mema. Muimbaji na Muundaji: Edwin Kamala Jina la Wimbo: WANIWAZIA MEMA Mwandishi wa Wimbo: Ernest E. Millinga Audio: Dr Keys Video: Paul Langu #WaniwaziaMema #EdwinKamala #Yeremia2911 #Nyimbozainjili #Mungunimwema