Tume ya mito yapendekeza kuhamisha wakenya wanaoishi kwenye ardhi inayopakana na mito jijini Nairobi

  • | K24 Video
    200 views

    Tume ya mito ya Nairobi inapendekeza kuhamisha wakenya wanaoishi kwenye ardhi inayopakana na mito muhimu jijini Nairobi. Hii ikiwa katika juhudi za si tu kuokoa umma kutokana na majanga kama mafuriko bali pia kupunguza uchafuzi wa mazingira kwani tume hiyo imetaja maeneo haya ya mabanda kuwa miongoni mwa sababu kuu za uchafuzi wa mito. Haya yanajiri wakati serikali ya kaunti ya nairobi imezuia uchimbaji kwenye ardhi kando ya mito na kusitisha idhini zote za ujenzi kufuatia mafuriko yaliyosababisha uharibifu mkubwa jijini.