Mozzart yachimba kisima wadi ya Nuu,Kitui

  • | K24 Video
    Tatizo la maji kwa wakaazi wa Kyumbi, wadi ya Nu ,  kaunti ya Kitui sasa limetatuliwa. Hii ni kufuatia uhisani wa kampuni ya Mozzartbet iliyowachimbia kisima cha maji. Kisima hicho kimegharimu shilingi milioni mbili na laki tisa na kinatarajiwa kufaidi zaidi ya familia 1000.