
193,363 views
2 Dec 2022
This song is a prayer inspired by Psalm 139:7-12, Ezekiel 47:3-5 and Phil 3:12 May grow to know God in a deeper way. #NIZAME Written by: Alice and Gideon Kimanzi Audio: Gydkym Music Bvs: Destiney Njeri, Eve Nyasha Ngoloma and Nelly Tuikong Lead guitar: Gloire Karume Bass guitar: Moise Basinza Video Director: Justin Mengere Social Media Posters & Reel: Eric Mayore (Crocsbassmahn) LYRICS Verse 1: Ni pahali gani pa kukimbia uwepo Wako eh? Nauliza ni wapi pa kujificha uso Wako Yahweh? Nikipanda mbingu (Wewe Upo) Nikishuka kuzimu (bado Upo) Nikijivika giza (We Waona) Hakuna mahali popote (We Haupo) Nataka nikujue unijuavyo Natamani nishike lile ambalo kwa ajili Yako nimeshikwa Chorus: Nataka nizame, nizame, nizame Kwa uwepo wako nizame, nizame Naomba Unifunike kwa Mbawa Zako Na tena Unijaze na Roho Wako Aaaah nizame Aaaah nizame Verse 2: Fikira Zako Baba (zina thamani kwangu) Maneno Yako Baba (yana thamani kwangu) Chunguza moyo wangu ili (Ujue mawazo yangu) Kagua njia zangu uniongoze (kwa njia za milele) Nikufahamu Unavyo nifahamu Natamani nishike lile ambalo kwa ajili Yako nimeshikwa Chorus: Nataka nizame, nizame, nizame Kwa uwepo wako nizame, nizame Naomba Unifunike kwa Mbawa Zako Na tena Unijaze na Roho Wako Aaaah nizame Aaaah nizame