
2,270 views
8 Jul 2020
Gospel Song. About How religion can change how we view God. Audio Producer: G-Law Production Video Director: Fidel Jilo Dancers: Abraham Masiga Isaac Busolo Peninah Fancy Jael Nabibia LYRICS 1. Nilikuona Mungu, Mungu mwenye hasira, Ungojaye nitende dhambi unimalize, Nikakuona Tena Mungu mwenye tamaa, Upendaye mfuko wangu kuliko nafsi yangu, nikang'ag'ana kutafuta hela, nikuletee usinilaani, nikang'ang'ana nikavaa magunia, Anga unione mtakatifu.... (Bridge) Huyo ni Mungu, Mungu wa dini, Hadi uliponifunza mwenyewe, Huyo ni Mungu, Mungu wa dini, Hadi uliponifunza mwenyewe, (CHorus) Kumbe wewe ni Mungu mwenye upendo uso na masharti, Unanyesha mvua yako kwa wenye dhambi na kwa wenye haki, Kumbe wewe ni Mungu ul'enifilia msalabani, kazichukua dhambi zangu ukazitupa mbali umenikubali, Upendo wako umenivuta karibu na wewe Upendo wako umenivuta karibu na wewe 2. Nikakuona Mungu mwenye kitabu kikubwa, Cha kuandikianga tu makosa ya watu, Nikakuona tena Mungu mwenye ghadhabu, Furaha yako kutufunza adabu, Nikang'ang'ana kukufurahisha, ila kila mara niligonga mwamba, Bidii yangu kumbe si kitu, Nikafa moyo wa kukuelewa, Huyo ni Mungu, Mungu wa dini ii Hadi uliponifunza mwenyewe ee Huyo ni Mungu, Mungu wa dini ii Hadi uliponifunza mwenyewe ee Kumbe wewe ni Mungu mwenye upendo uso na masharti, Unanyesha mvua yako kwa wenye dhambi na kwa wenye haki, Kumbe wewe ni Mungu ul'enifilia msalabani, kazichukua dhambi zangu ukazitupa mbali umenikubali, Upendo wako umenivuta karibu na wewe Upendo wako umenivuta karibu na wewe