
10,946 views
Kawira mwenye umri wa miaka 25, aliomba apatanishwe na mpenziwe Philip 30, ambaye wamekuwa na uhusiano tangia mwaka wa 2013. Mwanadada huyo alifichua kuwa alimuibia mpenziwe takriban elfu nne na alipokana, bwana Philip alimtishia kumpeleka kwa wachawi wa Kitui kama funzo. Kulingana na Kawira wawili hao hawakuwa wameshiriki mapenzi hadi mwaka huu ambapo alikubali. "Vile alinipeleka kwake akaniambia mkewe huja kwake na kuwa singetoka kwani wamama wa ploti wangeniona na hataki. Aliponiacha nikapata shilingi elfu nne nikajifichia. Nilipotoka siku ya Jumapili jana ndio alipofahamu kuwa fedha zilipotea alinitishia kuwa yeye ni mkamba wa kutoka Kitui na kuwa angenipeleka kwa wachawi. Sasa naomba anisamehe na akipenda turudiane. Nilijua ameoa lakini nilijua mkewe huishi mashambani kwani alitaka kunioa kama mke wa pili ila sikutaka." Alipopewa fursa bwana Philip alikubali kuwa Kawira alimuibia fedha ambazo ni elfu tano huku akidai kuwa alimuarifu amrudishie zile fedha kama ndiye aliyezichukua huku akipinga kuwa na mpango wa kumfanyia madhara ya uchawi. "Niliona hutanipea kwa hivyo nikaona nichukue kwani katoto kalikuwa kagonjwa lakini najua nilifanya makosa naomba msamaha." Alijitetea bi Kawira.