
26,611 views
Wengi hawakuwa na ufahamu walipoliskia jina lake leo asubuhi, lakini pindi tu msanii Evelyn Muthoka alipoanza kusimulia ushuhuda wake, aligusa nyoyo za milioni za wakenya wengi ambao wamepitia au wanapitia shida kama zake. Bi. Muthoka ni msanii wa nyimbo za injili na umaarufu wake ulianza kutamba tangia azindue kibao chake; 'Digital' ambacho kinawalenga sana vijana. Kando na kibao hicho, ana kanda kadhaa ambazo zimajumisha nyimbo kama; 'Shetani hauna mamlaka' 'kimbelele' na pia 'Adui yako msamehe'. Kando na nyimbo zake, masaibu aliyoyapitia bi. Muthoka ndiyo yaliyowagusa na hata kuwapa moyo waskilizaji wa Radio Jambo wengi wao ambao walikiri kuwa, huenda ikawa ndio mahojiano bora zaidi washawahi pata fursa ya kuskiza katika stesheni yetu kwa mda mrefu.