
310 views
Leo ikiwa siku ya Ijumaa, kama kawaita furahiday sisi huhothloliwa vi serious ndani ya studio na ndio maana huwa tunaalika wasanii wa nyanja mbalimbali iwe ni muziki au utumbuizaji. Hii leo msanii wa kike Fena Gitu ambaye anajulikana kwa nyimbo zake kama; 'African king' 'work' 'Far away love' na 'Jabulani' alitembelea studio zetu na pamoja na watangazaji Gidi na Ghost wakajibamba huku akisimulia yote kuhusu safari yake kama msanii. Anajitambulisha kama mwimbaji, mwandishi wa nyimbo na pia mtumbuizaji wa aina ya Urban Soul ikiwa ni mtindo unaounganisha ngoma za kizazi kipya mchanganyiko wa aina za Reggae, hiphop, rnb ma kadhalika muziki anaopenda kuuita 'Fenamenol'. Fena au ukipenda Fenamenol amelelewa katika famili ya kimuziki kwani akiwa mdogo aliimba kanisani na shuleni lakini alianza usanii kama taaluma mwaka wa 2008 huku akiwa msaidizi wa wasanii kama; Muthoni the drummer queen na Dela. Baadaye alirekodi kibao chake cha kwanza mwaka wa 2009 na hapo nyota yake ikaanza kung'aa kwani kufikia sasa ana kanda moja iliyo na nyimbo kumi na sita huku wimbo wake, 'Sema ng'we' ukiwa wimbo wake mpya. Lakini ni nini haswa humpa motisha anapoketi chini na kuamua kuandika wimbo? Kama 'Brikicho' 'sema ng'we' inanikumbusha tukiwa watoto kwani nililelewa Buruburu, kama msanii nikiandika wimbo sahii na i fananisha na maisha yangu kibinafsi, kwa hivyo saa zingine ni ubunifu au mambo yanayofanyika maishani mwangu kila siku. Skiza uhondo kamili kwani yalikuwa mahojiano ya kufana, huku akizumgumzia rais Kenyatta na mtindo wa usakataji rumba wa 'dab' ambao umezua mazungumzo tele katika mitandao ya kijamii.