
23,571 views
Je unamuamini mkeo au bwanako kiasi kwamba huwezi ficha siri yoyote kwake ikiwemo pia nambari ya siri ya akaunti ya benki? Basi hili lilibainika hapo jana wakti bwana Andrew alifichua kuwa mke wake alimuamini na nambari ya siri ya ATM na hapo ndipo alinyemelea na kutoa fedha za mkewe Mama Pauline, bila ruhusa. Andrew alikiri kuwa walikosana baada ya mkewe kugundua kuwa alikuwa ametoa fedha katika akaunti yake. Kulingana na Andrew shida ya ukosefu wa fedha za kulipa nyumba ndio iliyopelekea yeye kufanya yale. "Mke wangu alikuwa ameelekea kwa ATM na hapo ndipo aligundua kuna fedha haziko akanipigia simu na licha ya kumuahidi nitarudisha maradufu hataki maneno yangu, kila siku anapika anaweka chakula bila kuzungumza. Tangia Sunday hatusikilizani na haki ya ndoa sijapata jameni." Bi lilian alipopigiwa simu alifichua kuwa hiyo haikuwa mara ya kwanza mumewe kutoa zile fedha hata ingawa alikuwa na imani kuwa zile fedha zilikuwa pahala pazuri. "Isitoshe ile account ni ya mtoto na yeye hachangii kwa hii account mimi pekee ndio nachangia" Alijieleza mkewe Andrew. "Kitu yenye utafanya hatutaelewana mpaka urudishe hizo pesa. Mimi nimewacha maneno mengi na nimekusamehe lakini usiwahi toa fedha kwa account ya mtoto tena." Aliongeza mama Pauline akidai kuwa hataki mchezo na fedha ya mtoto kwani ni za siku za usoni. Pata uhondo kamili.