
71,088 views
Kweli aliyesema pesa ni sabuni ya roho kwa kweli hakuwa amekutana naye bwana Timothy ambaye aliwafurahisha wengi siku ya Alhamisi alipotangaza kuwa mapenzi yake kwa mpenziwe ni matamu na yenye maana kubwa kuliko mapenzi yake ya pesa. Timo mwenye umri wa miaka 35, aliomba apatanishwe na mkewe Judy wa miaka 26 ambaye walikosana mwaka uliopita. "Huyu mke wangu huwa tunakosanakosana kidogo anatoka anaelekea nyumbani, nikimchapa anatoroka kwani ana madharau hawezi ongea kwa heshima. Hajarudi wakati huu lakini huwa anakuja kupeleleza kama nimepata mke mwingine." Alieleza Timo ambaye pamoja wana watoto wawili katika ndoa ya miaka minne. "Siwezi rudi kwani amekuwa akinichapa kabisa na madharau mengi hata siwezi jieleza sahii. Tuna watoto wawili, mmoja ninaye naye alibaki na mwingine." Alisema Judy akisema hajapata mwanaume mwingine na hataki kupata mwingine kwani masaibu aliyoyapitia ndani ya ndoa ni machungu zaidi. "Naweza kusamehe lakini baada ya miaka mitano ijayo." Alisema Judy akidai kuwa kabla wawili hao wasameheane lazima wazazi wote wapatane kwani madharau yalianza kwa wazazi wake. Huku waskilizaji wengi wakihofia kuwa wawili hao hawangeweza kupatana licha ya juhudi zake bwana Gidi na Ghost Mulee, miujiza ikatokea ambapo Judy alilegeza kamba na kuahidi kumsamehe mumewe. "Judi nakupenda kuliko pesa!" Alisema bwana Timo akiwa na wingi wa furaha baada ya kusamehewa na mkewe. Pata uhondo kamili.