
889 views
Wakti seneta wa Elgeyo Marakwet, Kipchumba Murkomen alipozuru studio zetu leo asubuhi alizungumzia mengi kuhusu kazi yake kama wakili, mwakilishi wa watu kama seneta na pia maswala ya kisiasa. Jambo ambalo lilishtua na kufurahisha wengi ni wakati Murkomen alipofichua kuwa alihudhuria harusi ya aliyekuwa inspekta mkuu wa polisi, David Kimaiyo ambaye amejitokeza kumpokonya bwana Murkomen uongozi kama seneta wa Elgeyo Marakwet. "Bwana David Kimaiyo alikuwa hapa Radio Jambo na pia kule nje amekuwa akitangaza kuwa anataka kukuondoa kama seneta wa Elgeyo Marakwet, labda wazo lako ni lipi kuhusu azma yake na pia alisema hapa kwamba wewe umeshindwa na kazi." Gidi alimuuliza mheshimiwa. "Kwanza kabisa mwenye ameshindwa na kazi anajulikana na wakenya lakini ya pili sidhani kama itakuwa ya maana sana hapa katika redio tuongelee bwana Kimaiyo."Alisema Murkomen ambaye aliongeza kuwa wananchi walimuarifu kuwa asizungumzie kumhusu bwana Kimaiyo kwani yeye sio ajenda katika eneo la Elgeyo Marakwet. "Unajua, nyinyi muelewe Kimaiyo ni rika ya babangu na nililelewa kama kijana mdogo tukijua nyumba ya Kimaiyo ndio ile, alikuwa natubeba tukielekea shuleni na kwa sababu ni mzee na tuko kanisa moja na najua siku aliokoka akaja kanisani kufanya harusi, mie ndiye niliyeimba kwa harusi yake kwa hivyo itakuwa makosa kuongelea mzee wa rika ya babangu.. " Alifichua bwana Murkomen.