
8,760 views
Kumekuwa na mambo mengi kumhusu katika vyombo vya habari tangia alipokiasi chama cha kisiasa cha Jubilee na kujiunga na mrengo pinzani wa CORD, huku wengi wakibashiri ni yepi haswa yaliyochangia yeye kukimbilia 'Baba' (Raila Odinga). Na basi leo, aliyekuwa katibu wa chama cha TNA Onyango Oloo alitua studio zetu kufichua mengi kuhusu uhamiaji wake. Licha ya kukiri kuwa ana haki ya kikatiba kujiunga na kundi lolote la kisiasa, mojawapo ya yale bwana Oloo aliongelea kama sababu kuu ya kuhamia ODM ni Ufisadi ndani ya serikali ya Jubilee. Donda sugu ambalo limekuwa mada kila siku. "Baada ya kuchaguliwa kama serikali ya Jubilee baada ya mwaka mmoja tu tukaanza kuskia mambo ya ufisadi. Mara NYS tumeiba pesa nikasema haiwezekani. Usisahau nlikuwa msemaji wa chama tunafanya mkutano naletewa makaratasi naambiwa kuwa hayo yote yalikuwa porojo na nia ya upinzani kuangusha serikali." Alielezea Oloo. "Baadaye ikawa ni Eurobond, serikali ikaamka ikasema fedha zote zilitumika kwa njia safi kwa afya na kadhalika mimi na wenzangu wengine tulikuwa tunaamini hakuna ufisadi hii ni porojo ya upinzani kwani tuliwashinda sasa wanachuki. Lakini ukianglia asilimia 90 ya waliokuwa wanahusika walikuwa wanatoka mrengo mmoja wa muungano wa Jubilee, wakenya wanajua. Mda ukaenda, upinzani ukaweka moto mkali sana upande wetu mara Waiguru akijiuzulu baada ya mda mchache tukaanza upande wetu wakaanza kupigana na hapo tukagundua kuwa kuna siri ndani ya siri." Aliendelea kufichua jinsi alivyogundua kuwa kuna ufisadi mkuu ndani ya serikali iliyowahusisha wandani kadhaa. Waiguru anasema sio mimi pekee yangu nilibeba pesa kuna Kabura alibeba pesa na gunia, sijui Murkomen pia aangaliwe sijui bwana Duale pia akuje aongee sijui Farouk pia aongee, na ukikumbuka bwana Gidi kutokea wakati huo hamkusikia sauti yangu kwa sababu nilivunjwa moyo. Aliongeza bwana Oloo ambaye pia alifichua kuwa atawania kiti cha ubunge cha Kisumu ya kati kwani ameshawishiwa na wananchi. Nikasema heri nijiunge na wakenya wengine upande ule nihakikishe tumepigania haki ya wakenya pamoja na Raila Odinga ambaye amekuwa katika mstari wa mbele kupigania haki ya wakenya miaka hii yote ndipo mimi nikahama." Pata mahojiano yote kamili huku pia bwana Oloo akisema wazi timu za kandanda anazoshabikia humu nchini pamoja na Uingereza.