
4,405 views
Ukistaajabu ya Musa utaona ya firauni. Jamaa mmoja mjini Mombasa aliwashangaza wengi na vilevile kuingia katika vitabu vya kumbukumbu baada ya kulalamikia 'masaibu' anayopitia katika ndoa. Sote twajua kuwa kuna masaibu katika kila ndoa na basi malalamishi hutokea mara kwa mara lakini je, tangu lini mwanaume kalalamika kwa kupokea mapenzi tele kutoka kwa wake zao?. Kama bado unashangaa ni mwanaume upi mwenye uwezo huo basi tukio hili lilitokea Mombasa ambapo mwanaume mmoja alilalamikia mkewe ambaye amekuwa na tabia za kumsumbua kwa kummiminia mapenzi usiku kucha na mchana kutwa. Kulingana na usimulizi wake bwana Ghost Mulee, jamaa mmoja alikiri mapenzi ya mkewe hakuwahi yaona na alihofia kuwa yangemuua. Jamaa huyo ambaye ni mfanyikazi katika ufuo wa bara hindi alilalamika kuwa mkewe alikuwa na tabia ya kumpigia simu kila baada ya dakika tano kila siku akienda kazini, kumjulia hali na pia kumpa maneno matamu. Je ni wangapi amabao wanatafuta mapenzi kama haya huku nje?.