
825 views
Cheza nikaa umepigwa radi! Sidhani kuna wimbo mwingine ulioshika kasi zaidi nchini kuanzia mwaka uliopita huku watoto, wazee na hata wanasiasa wakiutumia mara kwa mara kwa ajili ya umaarufu wake. Huku wimbo huo wao Kymo na Stigah ambao ni wa ki injili ukiendelea kuvutia na kupendelewa na mashabiki wengi mwaka huu mpya, kuna jamaa mmoja ambaye milele atawalaumu wasanii hao wawili baada ya kisa kimoja cha kuchekesha na pia kuhuzunisha kutokea hivi maajuzi. Kulingana na Gidi ambaye alikuwa anasimulia kisa hicho kwa mwenzake, Ghost alidai kuwa huku nyimbo za injili zikitumiwa na wengi kuwapumzisha roho na kuwapa amani, jamaa huyo alikosa usaidizi na kupoteza mali yake kwa ajili ya wimbo huo. "Maeneo ya Githurai kuna jamaa mmoja amevamiwa na wezi sasa unajua wakati umevamiwa na wezi si unapiga nduru... uuuuwi uuuuwi sasa inasemekana wale majirani zake wanadhani anaimba huu wimbo sasa wanajibu Thitima! badala ya kusaidia jirani." Alisimulia Gidi huku Ghost Mulee akibingiria kwa kicheko chungu nzima.