
1,686 views
Siku ya jana watangazaji uwapendao wa kipindi cha Gidi na Ghost Asubuhi walikua na wingi wa furaha na uchangamfu tele, jambo ambalo tunalielewa zaidi haswa tukiwa katika msimu wa siku kuu ya Krismasi. Huku tukizihesabu siku zilizobakia ili wakristo wote duniani washerehekee siku ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo, Gidi kwanza alimpa mwenzake Ghost changamoto auimbe wimbo mmoja maarufu wa kusherehekea siku hiyo kuu, na isitoshe changamoto hiyo ilikuwa na zawadi ambayo ni takriban mia mbili. Lakini kile hakujua bwana Ghost ni kuwa mtego ulikuwa auimbe wimbo huo kwa lugha ya kihispania, na kama ulivyodhani Ghost ambaye ni gwiji wa lugha za kimataifa alishindwa na hivo kupoteza zawadi ile. Isitoshe Gidi alisimulia jinsi msikilizaji mmoja alivyotuma ujumbe akieleza kuwa ana ufahamu kidogo wa jinsi wananchi wa Tanzania wanavyo agiza vinywaji vya kileo kwa lugha mufti ya Swahili. Huku wa Tanzania wakijulikana kwa umaahiri wao katika lugha ile, msikilizaji yule alipeana mifano kadhaa ya kuchekesha huku Gidi akimwacha mwenzake Ghost mwenye wingi wa machozi ya furaha na kicheko, kila alipotafsiriwa majina yale ya vileo kwa lugha ya kiswahili. Kwa mfano kileo cha Johnie Walker cha tafsiriwa kama 'Yohana Mtembezi' huku kile cha Kenya Cane kikitafsiriwa kama 'Miwa ya Kenya'