
1,872 views
Hivi leo katika kitengo cha gumzo nao watangazaji Gidi na Ghost, wananchi walipewa fursa murwa kabisa kuangazia na kutoa mchango wao kwa kuangazia utendakazi wa serikali ya Jubilee, zaidi ya miaka mitatu tangu kuchaguliwa kwao. Haya yalijiri baada ya ripoti katika gazeti la The Star kuripoto kwamba Jubilee wameagiza makamishna wa kaunti zote nchini kuchambua na kuchukua maoni na malalamiko kutoka kwa wananchi, ili kubaini malalamishi yao kuhusu serikali kuu ili waweze kutengeneza kampeni za mwaka ujao. Hapo ndipo watangazaji hao waliwapa wananchi fursa ya kuichambua kwa kina utendakazi wa serikali kuu ya Jubilee ikiongozwa na Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake, William Ruto. Wananchi chungu nzima walipiga simu ili kupeana maoni yao huku wengi wakisifu miradi ya ku serikali kuongeza idadi ya wakenya wanaonufaika na umeme nchini. Wengine nao walilamikia visa vya ufisadi ambavyo vimekithiri humu nchini mojawapo ikiwa sakata ya NYS ikifuatiwa na sakata ya Afya ambapo mabilioni ya fedha zakisiwa kupotea. Katika pilkapilka za kutoa maoni yao, msikilizaji mmoja kwa jina Jared kutoka Maralal aliwachekesha wengi alipopiga simu kusifia mradi wa stima huku akiukashifu wakati huo huo. "Mimi ningewapa alama ya tano kwa kumi. Kwa sababu enyewe wamejaribu kuweka stima sasa hii stima ndio sijui utawekelea maji ya ugali kwa jiko halafu ukule nayo hiyo stima, kwa sababu ukiangalia watu wa Turkana wanaumia njaa, Kilifi njaa, Samburu njaa." Alisema bwana Jared.