
806 views
"Sipendi Ujinga" ni msemo ambao umepepea nchi nzima haswa katika mitandao ya kijamii. Msemo huu kawaida unatumika kama njia ya kuongeza ucheshi haswa kwa mambo makubwa inayowakumba wananchi. Leo pia wanajambo walitambua kuwa gavana Sospeter Ojaamong pia 'Hapendi Ujinga'. Hii ni baada ya gavana huyo wa Busia alipotangaza kuwa hatishwi wala hamna mpinzani yeyote aliye na uwezo wakumtisha katika nia yake ya kutetea kiti cha ugavana cha Busia, huku akiwashangaza wengi alipotangaza kuwa yuko tayari kutenga fedha kadhaa katika bajeti yake, ili kufadhili kampeni za wao hao wapinzani wake. We! moto kama pasi. Alitangaza hayo alipohudhuria mahojiano na watangazaji, Gidi na Ghost leo asubuhi huku akiwachekesha zaidi watangazaji hao. "Mheshimiwa inasemekana kwamba bwana Paul Otuoma amejitokeza pale, anataka kiti chako cha ugavana. Je uko tayari kupambana naye na je unahisi kwamba wananchi watakurudisha tena ama utang'olewa?" Aliuliza Gidi huku akitaka kujua msimamo wa gavana Ojaamong. "Kwanza lazima niseme kwamba Otuoma ni rafiki yangu, ni ndugu yangu na tumefanya naye siasa pamoja ingawa wengi wanataka kuleta uadui kati yetu. Ambayo hata haisaidii siasa si mwisho wa kila kitu urafiki na wandugu lazima waendelee. " Alijibu mheshiwa kabla ya kuongeza. "Nami nasema kama mkaaji wa kaunti ya Busia, wengi wajitokeze wasimame kama gavana na mimi nlipigania na Otuoma hakuwa. Lakini nasema mwenye anataka kusimama nitawasaidia hata kama huna pesa ya kusimama lakini una nia, nitawalipia. Nimesema angalau... hata wakose chakula lakini nitawasaidia ili wapambane nami wakinishinda nasema ndugu yangu chukua. Na kama hatakuwa (Otuoma) na pesa ya kusimama nitamsaidia, afadhali nitumie baiskeli." Aliongeza Ojaamong. Ni dhahiri hapendi ujinga.