
28,075 views
Kama kawaida katika kipindi cha Patanisho ukweli wamambo au uhondo kamili hubainika baada ya anayepatanishwa kusimulia masaibu yake wala si aliyetuma ujumbe. Haya yalibainika wazi wakti John 32, alipoomba apatanishwe na mkewe 26 ambaye kulingana na jamaa huyu walikosana miezi minane iliyopita. Wawili hao wamekuwa kwa ndoa kwa miaka minane na wamejaliwa mwana mmoja. John aliongeza kuwa shida kuu na ya kipekee ilikuwa ni tabia yake ya ulevi lakini ameasi tabia hiyo. Alisema hata baada ya mda huo wote ana imani bado mkewe hajapata mume mwingine na kuwa wangerudiana. Baada ya kumpigia Everlyn simu hapo ndipo kizaazaa kilipotokea na ukweli wote kufichuka huku mwanadada huyu akiwa na wingi wa hasira aliposimulia kuwa John alikuwa na njama ya kumchoma kabla ya wasamaria wema kumwokoa pindi tu alipomwagilia mafuta ya taa. Isitoshe alimtishia kuwa angekata kichwa chake na kunywa damu. "Nakwambia Radio Jambo ni wewe. Sitaki kuskia ukiniongelesha wewe ulikuwa unanimwagia mafuta halafu unanipeleka Radio Jambo, Usiku unaninyonga halafu unanipeleka kwa redio." Evelyn alimjibu bwana John huku akiwashangaza wengi akidai hizo ndizo sababu zilizomfanya atoweke kwao nyumbani. Licha ya juhudi za John kusema kuwa alikuwa amesingiziwa, mwishowe alikubali kuwa madai yote ni ukweli. Pata uhondo moto kama pasi katika kanda ifuatayo.