
16,831 views
Katika ndoa, licha ya mapenzi jambo moja ambalo nila muhimu zaidi ni uaminifu katika hali yoyote ile. Jambo hili lilibainika wazi hapo Maureen aliposimulia masaibi yake katika kitengo cha Patanisho akiomba apatanishwe na mume wake ambaye ni kana kwamba amemtenga. Kulingana na Maureen ambaye amekuwa kwa ndoa ya miaka 6 na mtoto mmoja, alikuwa na wingi wa majonzi huku akidai kuwa dunia ni kana kwamba imemfikia mwisho na angejitia kitanzi iwapo hangepatanishwa na mumewe Stephen. Alisema kwamba alimshughulikia mumewe kwa udi na uvumba huku akijikaza kisabuni wakti alipokuwa shuleni licha yake kutokuwa na kazi na mama wa mtoto wao mmoja. "Alipokuwa shuleni nlimshughulikia kwa kila kitu huku nikitumia fedha zangu kwake kwa matumaini kuwa tungesaidikia. Baada ya kutoka shuleni alisingiziwa amuoe mke ambaye amesoma na kuwa simfai. Alipopata kazi haungumzi nami kamwe na nateseka na mtoto wake pekee yangu." Alisema Maureen huku akiwa amejawa na uchungu mwingi. Bwana Stephen naye alijitetea akisema kuwa pia yeye amekuwa akiteseka kwani fedha anazopata haziwezi kumdumu pamoja na familia yake na pia wazazi wake kwani yeye ndiye kifungua mimba. "Nina deni kubwa sana la karo na pia ninapoishi maisha ni ya gharama ya juu zaidi ndio maanake shida hizi zote. Maureen ni mke wangu na ana mtoto wangu na baada ya mda mfupi tutasuluhisho yote." AlisemaStephen ambaye kwa sasa yuaishi Malindi huku mkewe akiwa nyumbani kwa mamake. Kwa wingi wa shaka, bibye Stephen alimuonya kuwa kuna magonjwa mengi humu duniani akimkumbusha kuwa amekuwa mwaminifu miaka hiyo yote na kuwa hangependa kuletewa magonjwa maishani mwake. Pata uhondo kamili.