
7,033 views
Ilikuwa ni kisa chungu nzima hapo jana wakti dada wawili Esther na Susan waliposhindwa kupatana miezi mitatu baada ya kukosana. Chanzo cha kukosana ni fedha ambazo zilizua matusi. Kulingana na Esther aliyeomba kupatanishwa na Susan, alimkopesha Susan fedha alizopata za chama. Baadaye mama anayemdai akaitisha fedha zake na baada ya kumwitisha Susan zile fedha alikasirika akisema kuwa stima zake haziwezi zimwa huku akiwa na fedha na hapo ndipo Esther alikasirika na kumuita dadake mkubwa 'Mwizi' na pia 'Mtoto'.