
2,434 views
Msanii mashuhuri wa kidini, Solomon Mkubwa alikuwa mgeni wetu siku ya Ijumaa, tarehe 11/11/2016 katika kipindi cha Gidi na Ghost Asubuhi katika kitengo cha waliobobea. Msanii huyu mzaliwa wa Congo anayejulikana kwa nyimbo kama Mfalme Wa Amani’ na ‘Niko wa yesu’ alisimulia chanzo cha jina lake, 'Mkubwa' jina la kipekee duniani. "Jina Mkubwa wakati nilipozaliwa katika familia nlikuwa na wale wazee watatu katika jamii. Mmoja alikuwa anaitwa MUlebo, mwingine Kulu mwingine Bwalite. Nlipozaliwa wazee wakasema lazima wangenipa jina." Alisimulia. "Yule Mulebo akanipa 'M' Kulu kanipa 'Ku' halafu Bwalite akanipa 'Bwa' ukiunganishe utapata jina 'Mkubwa' kwani wazee wote walinichangia majina yao na mungu amenijalia kuwa Mkubwa." kando na kuzungumzia maswala ya safari yake ya maisha na pia usanii, alizungumzia jinsi alivyo upoteza mkono wake wa kushoto, huku akidai kuwa kamwe hakuzaliwa mlemavu wala kapata ajali, bali kulingana naye ni uchawi ndio uliomfanya yeye kuupoteza mkono wake katika umri wa miaka kumi na miwili.