
4,754 views
Huku wapenzi wengi wakikosania mali, mipango ya kando na mambo ya vita ndani ya ndoa, bwana William alivunja 'mtindo' huo na kuharibu ndoa yake kwa tabia ya umbea ambapo alimhusisha mamake mzazi kumsengenya mkewe. Salalaa. William 31, aliomba apatanishwe na mkewe Christine 27, ambaye walikosana na akarudi kwao nyumbani baada ya kupandwa na mori huku William akisema alimuoa mkewe na watoto wawili na wakafanikiwa na mtoto mmoja pamoja.