
4,827 views
Wakati hali yako ya kimaisha haiambatani na jinsi mkeo anavyoishi basi ni dhahiri kuwa kutakuwa na msukosuko kwenye ndoa yenyu au hata kuleta kutoelewana na watu wengine. Nazungumzia hali tuliyoshuhudia asubuhi ya leo ambapo bwana Thomas aliomba apatanishwe na shemeji yake, Mike kisa na maana walikosana mda uliopita kwa kumpa bibiye pesa ambazo yeye mwenyewe kama bwanake hana uwezo wa kumpa. Kulingana na Thomas, Mike ambaye ni nduguye mkewe alikuwa na tabia ya kumtumia pesa mara kwa mara na swala hilo lilileta uwoga kwa roho yake, kwani alihofia mkewe atajawa na kiburi ndani ya nyumba na hivo kuharibu ndoa yake.