
10,428 views
Kwa wengi, jela ni mwisho wa maisha na pia mwisho wa maono lakini kwake bwana Peter Ouko, hukumu ya kifo kwake haikuichukulia kama mwisho wa chochote kwani alitumia nafsi hiyo kuto kata tamaa bali kama ngazi ya kufikia lengo lake la maisha. Kulingana na Ouko masaibu yake yote yalianza mnamo Disemba tarehe kumi na tisa mwaka mwa 1998 ambapo mkewe Jennifer hakurudi nyumbani na katika juhudi zake za kumtafuta mkewe usiku wa giza, aligundua kuwa mkewe alikuwa ameuawa mtaani Buruburu.