
5,531 views
Leo ikiwa siku ya kimataifa ya mtoto aliye na jinsia mbili, katika kipindi cha Gidi na Ghost Asubuhi tulikuwa naye Gathoni Muchomba ambaye ni mwanaharakati wa watoto walio na na hali hiyo, pamoja na Sidney kijana ambaye alizaliwa akiwa na hali ile. Kulingana na wazazi wake Sidney, walikuwa na bado wana imani kuwa alizaliwa akiwa mtoto wa kike kinyume na alivyojihisi. Sidney alisimulia jinsi alivyogundua yeye ni mwana wa kiume lakini sio wa kike akiwa na umri wa miaka kumi na mitatu, na hapo ndipo shida nyingi zilianza kumfuata huku wazazi wake wakigeuka kuwa wanyama.