
349 views
Mheshimwa Kalonzo Musyoka asubuhi ya leo alikanusha madai ya seneta wa Machakos, Johnson Muthama kwamba muungano wa CORD tayari umeamua nani haswa atakayepeperusha bendera ya urais mwaka ujao. Takriban wiki moja iliyopita, Seneta Muthama alidokeza hayo alipokuwa akihojiwa ndani ya Radio Jambo. Nataka kuwaambia wananchi kuwa tunashindana na serikali ambayo ina pingu, pesa na vyombo vya uongozi. Ikiwa miezi hii kumi na moja iliyobaki tutaweza kumtoa kiongozi au kinara wetu, Jubilee watamtoboa tumbo hata kabla hajatoka ndani ya nyumba.” Alisema Muthama.