
9,909 views
"Mimi na bwanangu mheshimiwa Mungatana hatukupatana barabarani! Alito kijasho kunipata" mwanahabari mashuhuri nchini, Mwanaisha Chidzuga alisimulia wakti alipokuwa akihojiwa na mtangazaji wa bustani la MJ, Maureen Massawe Jappani. Mwanaisha ambaye ni mkewe mwanasiasa aliyekuwa mbunge wa Garsen, Danson Mungatana alisimulia jinsi wawili hao walivyopatana huku akifichua kuwa safari ya Mungatana ambaye anajulikana kama 'mla mamba' kujishindia roho ya mpenziwe, haikuwa tu mteremko wa halua na asali bali ilihusisha bidii chungu nzima na jasho si haba. "Kwa hivyo hamkupatana kwa chumba cha habari?" Aliuliza Massawe.