
453 views
Ghost Mulee ambaye anajulikana kama '''mzee wa nyumba' katika kipindi cha Gidi na Ghost Asubuhi, alitoa pendekezo ambalo tayari limewafurahisha wengi huku likiwakera wengine vile vile. Kulingana na Mulee, kamwe mwanaume haswa mabwana hawafai katika hali yoyote ile kuwekelea hata kidole kwa wake zao wanapokosana. Hii ilikuwa baada ya kipindi cha patanisho ambapo waskilizaji walitibiwa na dawa ya kicheko baada ya wapenzi wawili James na Rose kusameheana, lakini kisa kilitokea wakti James alikiri kuwa ana hofu ya kwenda kwa mkewe kumchukua kirasmi kwani licha ya kuwa hajalipa mahari, alihofia kupokea kichapo cha mbwa kutoka kwa jamii ya mkewe kwa kumpiga.